Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

unyonyeshaji watoto

© UNICEF/Zahara Abdul

Maziwa ya ng'ombe yana protini isiyoweza kumeng'enywa kwenye tumbo la mtoto mwenye umri wa chini ya miezi 6 - Mtaalamu

Ni mwaka mmoja tangu mradi wa mafunzo kuhusu lishe endelevu ulipoanzishwa mkoani Morogoro kwa ufadhili wa shirika la Save the Children na shirika la Marekani la msaada wa kimataifa USAID. Sehemu ya mradi huo ni kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa halisi ya mama angalau kwa miezi sita ya kwanza. Je, wanuafaika wa mradi huo wanasemaje? Wameelimika kwa kiasi gani tangu mradi huo kuanzishwa mwezi Agosti mwaka jana 2019? John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM amezungumza nao na kuandaa makala hii. 

Sauti
3'25"
UN

Vyakula vya watoto wenye umri wa chini ya miezi 6 vina sukari nyingi- Ripoti

Tafiti mpya mbili zilizofanywa na shirika la afya ulimwenguni, WHO kanda ya Ulaya zimebaini kuwa vyakula vinavyotangazwa kwa ajili ya watoto wenye umri wa chini ya miezi sita vinakiuka kanuni na vina kiwango cha  sukari kupita kiasi. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.

Tafiti hizo zimefanywa kwa kukusanya takwimu kutoka vyakula au vinywaji 7955 vinavyouzwa kwa ajili ya watoto wachanga kutoka maduka 516 kwenye miji 4 ya Vienna, Austria; Sofia, Bulgaria; Budapest, Hungary; na Haifa, Israel kati ya mwezi November mwaka 2017 hadi mwezi Januari mwaka jana wa 2018.

Sauti
2'4"