UNWomen

Zanzibar inasonga kuwawezesha wanawake vijijini: Fatma Bilal

Serikali ya Zanzibar imekuwa mfano wa kuigwa katika suala la uwezeshaji wanawake vijijini kujikwamua na umasikini kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo kama ilivyo  katika ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. 

Kongamano la wanawake laendelea Sudan Kusini

Wakati kamisheni ya wanawake kutoka ulimwenguni kote, ya CSW62 ikiendelea jijini New York, mjini Juba nchini Sudan zaidi ya wanawake 150 wawakilishi wa jamii mbalimbali wamejumuika katika kongamano la kitaifa  la siku 3 kujadili amani na usalama nchini humo.

#Metoo ni chachu ya kukomesha ukatili kwa wanawake: Bi Mohammed

Mkutano wa kamisheni ya  hali ya wanawake duniani ,CSW62 unaendelea  mjini New York, ukisheheni mitazamo mbalimbali kutoka kwa washiriki akiwemo naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed ambaye yuko mstari wa mbele kuunga mkono kampeni ya #Metoo ilizoanzishwa na wanawake Wakimarekani baada ya kubaini unyanyasaji wa kingono unaofanywa na wanaume wenye madaraka.

Kuanzia majumbani hadi vyumba vya mikutano tuweke usawa- Guterres

Akizungumza katika ufunguzi wa kamisheni hiyo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amesema huu ni wakati muhimu kwa kuhakikisha madaraka na usawa unamfikia mwanamke na hususani wa Kijijjini ambaye amekuwa akisahaulika

Sauti -
2'1"

Madaraka na usawa vimfikie mwanamke- Guterres

Mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Maudhui ya mkutano huo wa wiki mbili ni changamoto na fursa katika kufikia usawa wa jinsia na kuwezesha wanawake na wasichana waishio vijijini. 

12 Machi, 2018

Jaridani hii leo CSW62 yafungua pazia, wanawake na wasichana wa vijijini wapatiwa kipaumbele. Washiriki kutoka Kenya na Tanzania nao wapaza sauti. Kwenye makala tunaenda Burundi kuangazia mazingira na bila kusahau ushauri kwa nchi zinazokabiliwa na vita.

Sauti -
11'39"

CSW62 yaanza leo New York

Zaidi ya washiriki 8000 wanahudhuria mkutano huu wa wiki mbili na kinachoangaziwa zaidi ni mustakhbali wa mwanamke na msichana wa kjijini.

IOM itasimama kidete na wanawake wahamiaji popote walipo

Ikiwa leo  ni maadhimisho ya siku ya wanawake dunia, Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, limesema litasimama kidete  kumtetea na kumlinda kila mwanamke au msichana mhamiaji mwenye moyo wenye  wa matumaini, akili iliyojaa mawazo ya maendeleo popote alipo duniani.

UN iwe mfano kutekeleza usawa wa jinsia- Guterres

Wahenga walinena kuwa toa kwanza boriti kwenye jicho lako na ndio utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako na ndilo jambo ambalo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameamua kufanya katika kupigia chepuo usawa wa kijinsia!

07 Machi 2018

Nchi nyingi hazina takwimu kuhusu watoto, hivyo SDGs mashakani. Nchini Tanzania UN Women na harakati za kukwamua wanawake. Mkuu wa shule ya Weru Weru nchini Tanzania ataja lengo la SDGs analopatia kipaumbele,  na makala twaenda DR Congo, wasichana wakimbizi wasakata kabumbu. 

Sauti -
11'6"