Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

UNPFII

Kulet Adam Ole Mwarabu kiongozi wa jamii ya kimaasai kutoka Tanzania, akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
UN News

Licha ya changamoto Tanzania haijawapa kisogo watu wa jamii za asili: Adam Ole Mwarabu

Jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa jamii za asili kikao cha 24 UNPFII, limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani na kandoni mwa jukwaa hilo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki ambaye ni kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu, wamejadili mengi kuanzia maendeleo hadi ujumuishwaji wa jamii za asili. Ambapo amesema taifa hilo la Afrika Mashariki halijazipa kisogo jamii hizo.

UN News/Sharon Jebichii

Kutimiza azimio la watu wa jamii za asili ni jukumu la mataifa yote duniani - Adam Ole Mwarabu

Jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa jamii za asili limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kandoni mwa jukwaa hilo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu, wamejadili mengi lakini Ole Mwarabu anaanza kwa kukumbusha alichokibeba kwenye jukwaa la mwaka jana kinavyotekelezwa nchini mwake.

Sauti
6'48"

08 MEI 2025

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ambayo Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuzungumza na kiongozi wa kijamii kutoka Jamii ya wafugaji ya Wamaasai mkoani Morogoro nchini Mashariki mwa Tanzania Adam Kulet Ole Mwarabu.

Sauti
11'12"

06 MEI 2025

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa makao makuu ambako Idhaa hii Dokta Willis Ochieng kutoka Kenya aliyehudhuria ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kilimo na maendeleo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani tunakwenda Ghana.

Sauti
12'3"
UN News/Sharon Jebichii

Maoni kutoka washiriki kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria mkutano wa jamii za asili UNPFII

Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili, ukileta pamoja washiriki kutoka maeneo mbalimbali kote duniani. Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na baadhi yao.

Sauti
3'24"

30 APRILI 2025

Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa mpox, na walinda amabini wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo. Makala inamuulika siku siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz namashinani tunasalia hapa makao maku kusikia ujumbe wa mwakilishi wa shirika la watu wa jamii za Asili.

Sauti
11'14"

29 APRILI 2025

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkoa wa Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ambapo vijana wameshika hatamu kuboresha mustakabali wao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari  na mashinani tunasalia hapa makao makuu.

Sauti
11'44"

25 APRILI 2025

Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa DRC waliokimbilia Burundi, na ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia ugonjwa wa malaria na mashinani tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili.

Sauti
10'57"