UNOC3: Hatuwezi kuacha uroho uamue hatma ya dunia yetu asema mkuu wa UN
Bahari iko hatarini na uroho ndio chanzo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo akizungumza na waandishi wa habari huko Nice Ufaransa.
Bahari iko hatarini na uroho ndio chanzo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo akizungumza na waandishi wa habari huko Nice Ufaransa.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika ukanda wa Gaza, huko mashariki ya Kati kwenye eneo la Palestina lialokaliwa kimabavu na Israeli ambapo vinazidi kuibua changamoto mpya kila uchao.
Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa hii.
Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini.
Tarehe 9 Juni, wajumbe kutoka kote duniani watakutana katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3), mjini Nice, Ufaransa, ili kuharakisha hatua na kuhamasisha wadau wote kulinda na kutumia bahari kwa njia endelevu.