UNICEF

Machafuko yalazimisha watoto 600,000 kukosa elimu Cameroon:UNICEF

Zaidi ya asilimia 80 ya shule zimefungwa katika majimbo ya Kaskazini Magharibi na Kusini magharibi mwa Cameroon kufuatia machafuko yanayoendelea na kuwalazimisha watoto zaidi ya 600,000 kukosa fursa ya elimu  limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Mtu 1 kati ya 3 duniani hana fursa ya kupata maji safi ya kunywa na huduma za kujisafi- UNICEF/ WHO 

Ripoti mpya kuhusu pengo la usawa katika fursa ya kupata maji safi ya kunywa na masuala ya usafi  na kujisafi inaonyesha kwamba zaidi ya nusu ya watu wote duniani hawana fursa ya kupata huduma salama za usafi.

Asilimia 61 ya watu Sudan Kusini kukabiliwa na janga la chakula:WFP/FAO/UNICEF

Mamilioni ya watu nchini Sudan Kusini kukabiliwa na janga kubwa la ukosefu wa chakula kuwahi kutokea nchini humo yameonya leo mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa yakihimiza hatua kuchukuliwa haraka.

UNICEF yadhamiria kunusuru watoto dhidi ya Ebola Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limezindua mkakati kwa kukabiliana na Ebola nchini Uganda kufuatia kuthibitishwa kwa visa vitatu ikiwemo vifo viwili Magharibi ya nchi hiyo

Dunia imeshindwa kupatia huduma bora za uzazi wajawazito maskini- UNICEF

Tathmini mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF inaonesha kuwa zaidi ya kaya milioni 5 barani Afrika, Asia na Amerika ya Kusini hutumia zaidi ya asilimia 40 ya matumizi yao yasiyo ya chakula katika huduma za afya ya mama mjamzito kutokana na gharama hizo kuwa za juu.

Familia moja nchini Kenya yarejesha ndoto ya masomo kwa mkimbizi kutoka Burundi

Nchini Kenya, mradi wa pamoja wa Muungano wa Ulaya na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na shirikisho la makanisa ya kilutheri duniani, umesaidia kulinda wakimbizi watoto kwenye kambi ya Kakuma nchini Kenya baada ya kukimbia  madhila katika nchi zao. 

Mtoto 1 kati ya 7 duniani kote huzaliwa na uzito mdogo kupindukia- Ripoti

Takwimu mpya zilizotolewa leo na watafiti kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa na Chuo cha tiba za kitropiki na afya cha London, Uingereza zimeonyesha kuwa mwaka 2015 zaidi ya watoto milioni 20 walizaliwa duniani kote wakiwa na uzito wa chini kupindukia, ambao ni chini ya kilo mbili na nusu au pauni 5.5

Takriban watoto 900 waachiliwa huru na makundi yenye silaha Nigeria:

Watoto takriban 900 waliokuwa wakishikiliwa na makundi mbalimbali yenye silaha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wameachiliwa huru na makundi mbalimbali yenye silaha na kufanya idadi ya walioachiliwa na makundi hayo tangu mwaka 2017 kufikia zaidi ya 1700. 

Ulinzi wa haki ya mtoto ni msingi wa mafanikio ya mkataba wa amani CAR- Gamba

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye mizozo, Virginia Gamba amehitimisha ziara  yake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR akisema usaidizi madhubuti kwa wavulana na wasichana walioathirika na mzozo nchini humo ni jawabu mujarabu la kufanikisha mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi Februari mwaka huu. 

Zaidi ya watoto 300,000 raia wa Venezuela walioko Colombia wanahitaji msaada wa kibinadamu: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema linasaka dola milioni 29 ili kuongeza bajeti yake ambayo kwa sasa ni takribani dola milioni sita tukwa lengo la kuwasaidia maelfu ya Watoto wa Venezuela wanaoishi nchini Colombia.