Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

UNGA80

UN News/Abdelmonem Makki

Akiwa Doha, Rais wa Baraza Kuu aona watoto wa kipalestina walivyo na matumaini licha ya zahma walizopita

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock ametembelea wakimbizi wa kipalestina huko Doha nchini Qatar kuwajulia hali na kujionea maisha yao baada ya kuondolewa wakati wa vita kali huko Ukanda wa Gaza eneo la wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel na kuletwa nchini Qatar kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Leah Mushi anatupa taswira ya ziara yake hiyo.

Sauti
4'6"
Omon Ukpoma-Olaiya Kiongozi wa Timu ya Uwekezaji ya UNCDF ya Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini na Mataifa ya Kiarabu akihojiwa na Anold Kayanda huko New York, Marekani (Sept 2025)
UN News

Namna UNCDF ilivyosaidia jamii kupata mtaji na huduma muhimu Rwanda, Burundi, Malawi na Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Mitaji, UNCDF, limeendelea kuwekeza katika kupunguza hatari za hasara za kifedha na kufungua fursa za mitaji nafuu kwa vijana, wanawake na sekta muhimu barani Afrika. Hayo yanasemwa na Omon Ukpoma-Olaiya, Kiongozi wa Uwekezaji wa UNCDF kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Kusini na Nchi za Kiarabu, alipokuwa akizungumza na Anold Kayanda na Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofikia tamati Septemba 29, 2025.

Picha ya Crest ya Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Mkutano Mkuu.
UN Photo/Loey Felipe

Takwimu za UNGA: Hotuba ndefu zaidi, Wanawake Wachache, na baadhi kutokuwepo

Kwa muda wa siku sita, safu ya viongozi wa dunia (194 kwa jumla, 24 tu kati yao wakiwa ni wanawake) walitoa hotuba kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutoka kwenye jukwaa lake la kuvutia la marumaru ya kijani kibichi, wakiangazia vita huko Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, DRC, Sudan, Gaza na Ukraine, mzozo wa mabadiliko ya tabianchi, na mageuzi katika Umoja wa Mataifa, miongoni mwa masuala mengine mengi muhimu.

UN News

EAC yasisitiza usalama, uchumi na masuala ya kidijitali katika Mjadala Mkuu wa UNGA80

Kama unavyofahamu Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 umekunja jamvi rasmi  jana Jumatatu. Na tumepata fursa ya kuzungumza na washiriki mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa mjadala huo kuangazia mchango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutekeleza ajenda ya Umoja wa Mataifa ikiwemo masuala ya Amani na usalama, maendeleo na ushirikiano wa kikanda. Ungana nao.

Sauti
9'11"

30 SEPTEMBA 2025

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa UNGA80. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.

Sauti
12'3"