UNGA73

Ugonjwa wa TB si kulogwa, muhimu ufuate masharti ya matibabu -DJ Choka.

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuwa ugonjwa wa Kifua Kikuu  ndio unaongoza kwa kuwa ugonjwa hatari zaidi wa kuambu

Sauti -
3'27"

Hatua kali ni lazima katika kuzuia kuenea silaha za maangamizi-SC

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametaka mshikamano na hatua kali kutoka kwa baraza hilo dhidi ya silaha za maangamizi zikiwemo za nyuklia, kibaolojia na za kemikali.

Uchaguzi utafanyika mwaka huu DRC kama ilivyopangwa:Kabila

Uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu hautobadilishwa utafanyika kama ilivyopangwa.

Afrika tumieni fursa ya biashara huru kukuza viwanda na uchumi:UNIDO

Katika miongo michache ijayo Afrika imeelezwa itakuwa bara changa na lenye watu wengi zaidi duniani , huku idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi ikitarajiwa kuongezeka na kufikia milioni 450 sawa na asilimia 70 ifikapo mwaka 2030.

Bado haki za binadamu zimesalia ndoto kwa wakazi wengi duniani- UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema miaka ya 70 ya tamko la haki za binadamu duniani, haijawa tiketi kwa kila mtu kufarahia haki za msingi zilizoainishwa katika nyaraka hiyo.

Kutobaini mapema na kutibiwa TB ni mtihani mkubwa Afrika:WHO

Fursa ya kutopimwa mapema, kugundulika na kupata matibabu yanayostahili ya ugonjwa wa kifua kikuu ndio mtihani mkubwa wa mapambano ya vita dhidi ya ugonjwa huo barani Afrika. 

Marekani inaendeshwa na wamarekani: Trump

Marekani inaendeshwa na Wamarekani na ukiheshimu uhuru wetu hatutokuingilia wala kukwambia la kufanya. Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Marekani Donald Trump alipouhutibia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Sauti -
3'19"

Vijana wa sasa si wa kusubiri kufunguliwa milango- Rais Ramaphosa

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amehutubia mjadala mkuu wa Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo akisema kuwa vijana wa sasa si wale wa kusubiri kufunguliwa milango.

Je Afrika ni tishio kubwa? Ahoji Rais Mutharika

Malawi imesema inaunga mkono msimamo wa Afrika wa kutaka kuwepo kwa wajumbe wawili wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na 5 wasio na kura turufu.

Naona mustakabali mkubwa ambao unaongozwa na vijana-Restless Development

Umoja wa Mataifa Jumatatu hii umezindua mkakati wake mpya kuhusu vijana ukilenga kuimarisha mchango wa takribani vijana bilioni 2 duniani  kwa lengo la  kukuza amani, uadilifu pamoja na kuwa na  dunia endelevu. Mkakati huo umepatiwa jina,  “Vijana 2030:Mkakati wa  Umoja wa Mataifa  kwa vijana,” 

Sauti -
3'48"