Umeme wa sola washika kasi Tanzania, UNDP yaonyesha njia
Lengo namba 7 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015, yanataka pamoja na mambo mengine kuhakikisha nishati ya kisasa iliyo nafuu na ya uhakika inapatikana ili kufanikisha shughuli za kila siku za maendeleo. Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la mpango wa maendeleo, UNDP limeamua kuonyesha njia kuwa hilo linawezekana kwa kuwa kuwekeza kwenye sola mwanzoni ni gharama lakini ni gharama inayopunguza gharama za usoni.