Chukua hatua sasa kwa ajili ya Afrika yenye mnepo tunayoitaka: UNDRR
Jukwaa la tisa la Kikanda la Afrika kwa ajili ya Kupunguza hatari za majanga linaendelea mjini Windhoek, Namibia, likiwa na kaulimbiu ya "Chukua Hatua Sasa kwa Ajili ya Afrika Yenye Mnepo Tunayoitaka." Mkutano huu wa siku nne umeandaliwa na serikali ya Namibia kwa kushirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza hatari za majanga (UNDRR) na Kamisheni ya Umoja wa Afrika, kwa ushirikiano na Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).