Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Ján Kubiš amelaani shambulio la bomu lilitokea huko Tirkit kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Ukatili uliofanywa na waasi wa ISIL Iraq ni wa kutisha na unaweza kuwa ni uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu, imesema leo ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa.