unama

Afghanistan fanyeni uchaguzi ulio huru na wa haki:UNAMA

Ujumbe wa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umepongeza hatua ya tume ya uchaguzi nchini humo IEC kutangaza ratiba ya uchaguzi wa rais ambao umepangwa kufanyika mwezi julai mwaka wa 2019.

Acheni mashambulio dhidi ya raia mjini Kabul: UNAMA

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulio ambalo limetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la mji mkuu Kabul na kusababisha vifo na majeruhi.

Licha ya ghasia, waafghanistani wana ‘kiu’ ya amani- UNAMA

Mkutano wa kimataifa wa ngazi ya juu umeanza leo  huko Geneva, Uswizi ukilenga kuonyesha mshikamao na wakazi wa nchi hiyo iliyogubikwa na vita na pia kusaidia serikali katika harakati zake za kuchagiza maendeleo sambamba na amani na usalama.

Licha ya machafuko UN yataka wapiga kura kuhakikishiwa haki yao Afghanistan

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA unasema licha ya uchaguzi wa bunge hii leo kughubikwa na ghasia umetiwa moyo na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza  kutekeleza haki yao ya msingi ya kupiga kura na kutaka hakikisho kwa wote kuweza kupiga kura.

Raia waendelea kuwa chambo mzozoni Afghanistan- Ripoti

Wananchi wa Afghanistan wameendelea kuwa waathirika wa mapigano yanayoendelea nchini mwao ambapo idadi kubwa wameendelea kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mashambulizi yanayofanywa hususan na wapinzani wa serikali.

Wanaoshambulia raia Afghanstan lazima wawajibishwe:UNAMA

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan , (UNAMA) umeshutumu mfululizo wa mashambulizi ya mabomu hii leo katika jimbo la Nangarhar mashambulizi ambayo yameua takribani raia 21 na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa, na kusema unatiwa hofu na mashambulizi hayo ambayo yanawalenga raia na shule.

Sherehe za Eid zaleta ahueni kwa wananchi wa Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umekaribisha  tangazo la serikali nchini humo la kusitisha mapigano bila masharti  yoyote kwa ajili ya sherehe za Eid El Haj, na hivyo umetoa wito kwa pande kinzani kwenye mzozo kutumia fursa hiyo kukomesha ghasia.

UN iko bega kwa bega na Afghanistan katika michakato ya chaguzi

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, umekaribisha hatua ya tume huru ya uchaguzi  nchini humo, IEC ya kutangaza kuwa uchaguzi wa rais utafanyika tarehe 20 Aprili mwaka ujao wa 2019.

Watu 13 wauawa Afghanistan, UN yalaani

Watu 13 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la kujilipua lililofanyika leo huko Jalalabad nchini Afghanistan.

Kuchagiza amani Afghanistan ni wajibu wa kila mwananchi: UN

Kila hatua inayopigwa kuelekea amani nchini Afghanistan ni muhimu sana kwa sasa kulliko wakati mwingine wowote ulee. Wito huo umetolewa leo na  viongozi wa kijamii katika mdahalo unaoungwa unaofanyika mkoa wa Kusini wa Kandahar nchini humo na kuungwa mkono na Umoja wa wenye  lengo la kumulika mbinu za kutanzua mgogoro na kujenga mshikamano wa jamii.