Kanda zote ziko nyuma katika kudhibiti kuenea kwa Ukimwi na mafanikio makubwa tuliyopata kwa watoto hayahifadhiwi huku wanawake ndio wanaoathirika zaidi, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI-UNAIDS, Michel Sidibe, wakati wa uzinduzi wa ripoti mpya ya hali ya UKIMWI duniani hii leo.