Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umetangaza hatua mpya katika kusaidia juhudi zinazoongozwa na serikali ya Sudan kusini katika kuzuia na kujiandaa na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19.
Ingawa watoto hawana jukumu kubwa katika vita, mamilioni miongoni mwao wanajikuta katikati ya machafuko ambayo sio watazamaji bali walengwa, umesema Umoja wa Mataifa ukizinfdua muongozo wa kuwalinda watoto katika hali za vita.
Salamu za pongezi ya siku ya kuzaliwa zimetumwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa 5 wa Umoja wa Mataifa Javier Pérez de Cuéllar kwa kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema ameshtushwa na kuhuzunishwa sana kuanguka kwa ndege ya abiria ya Ukrain hii leo Jumatano karibu na mji mkuu wa Iran Tehran.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake na kutoa wito wa kupunguza mvutano katika eneo lote la Ghuba baada ya kuuawa kwa jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani nchini Iraq.