Uchumi wa dunia unaweza kushuka kwa asilimia 0.9 mwaka huu wa 2020 kutokana na janga la virusi vya Corona, COVID-19, na uzalishaji wa dunia utashuka hata zaidi endapo vikwazo vya kiuchumi vitaendelea katika robo ya tatu ya mwaka huu, na kama bajeti za kupambana na janga hili hazitosaidia kipato na wateja, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo Jumatano na Umoja wa Mataifa.