UN

Kuna haja ya kujikita na waathirika wakubwa wa mzozo wa Sudan Kusini:UN/AU

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika AU ambao uko ziarani Sudan Kusini kwa siku tatu, umeonyesha mshikamano wake na watu pamoja na uongozi wa nchi hiyo ukisema uko tayari  kuunga mkono mkataba wa amamani uliotiwa saini hivi karibuni mjini Addis Ababa.

Heri nusu shari kuliko shari kamili ya mabadiliko ya tabia nchi:UN

Mtihani wa mabadiliko ya tabia nchi ni mkubwa lakini ni wajibu wa kila mtu na kila nchi kuchukua hatua sasa kuepuka janga lenye gharama kubwa hapo baadaye, umeonya Umoja wa Mataifa. Kiwango cha joto kinaongezeka  na athari ni pamoja na haki za binadamu za afya, chakula, maji na mazingira.

Sauti -
2'29"

08 Octoba 2018

Jarida la leo Jumatatu 08/10/2018:

- Mabadiliko ya tabianchi yaathiri haki mbalimbali za mwanadamu;

- UNPA na kampeni dhidi ya Fstula sudan Kusini;

- Uganda yaanzisha kampeni dhidi ya kifua kikuu TB

Sauti -
11'34"

Teknolojia mpya ina manufaa ikitumika ipasavyo-Utafiti wa UN

Ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu teknolojia mpya imesema nishati itokanayo na vyanzo visivyoharibu mazingira hadi plastiki zinazooza kwa urahisi, akili bandia na magari ya umeme, vina mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wanadamu hususani katika kusongesha jitihada za kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na kuangazia mabadiliko ya tabia nchi.

Kuna haja ya kujikita na waathirika wakubwa wa mzozo wa Sudan Kusini:UN/AU

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika AU ambao uko ziarani Sudan Kusini kwa siku tatu, umeonyesha mshikamano wake na watu pamoja na uongozi wa nchi hiyo ukisema uko tayari  kuunga mkono mkataba wa amani uliotiwa saini hivi karibuni mjini Addis Ababa.

Misaada ya kibinadamu na maendeleo vinapaswa kwenda pamoja-UN

Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Achim Steiner na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock, hii leo Oktoba 7 wameikamilisha ziara yao ya kwanza ya pamoja nchini Chad.

Jitihada zaidi zinahitajika kulinda haki ya kukusanyika na kujumuika Tunisia- Mtaalamu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za mikusanyiko ya amani na kujiunga na vyama, Clément Nyaletsossi Voule, ameridhishwa na jitihada za serikali ya Tunisia za kuimarisha demokrasia tangu yalipofanyika mapinduzi mwaka 2011 huku akizisihi mamlaka hizo kuongeza jitihada kulinda haki za mikusanyiko ya amani na kujumuika.

UN, AU na Sudan wakubaliana kuhusu mustakhbali wa UNAMID Darfur

Umoja wa Mataifa, UN, Muungano wa Afrika, AU pamoja na serikali ya Sudan wamekubaliana kwa pamoja kuendelea kutekeleza makubaliano ya pamoja ya kuwezesha ujumbe wa pamoja wa wa UN na AU wa kulinda amani Darfur, UNAMID kuendelea kutekeleza majukumu yake wakati huu ambapo unajiandaa kuhitimisha shughuli zake.
 

Sudan Kusini tunapiga hatua,asanteni sana- Gai

Mwaka jana nilisimama mbele yenu nikiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi iliyogubikwa na vita. Leo hii nimesimama tena mbele yenu kama shuhuda wa kile ambacho wanachama wa chombo hiki adhimu wamesaidia kufanikisha ndani  ya Jamhuri ya Sudan Kusini.

Sauti -
2:56

Sudan Kusini ya mwaka jana si ya mwaka huu, shukrani UN, AU na wadau- Gai

Mwaka jana nilisimama mbele yenu nikiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi iliyogubikwa na vita. Leo hii nimesimama tena mbele yenu kama shuhuda wa kile ambacho wanachama wa chombo hiki adhimu wamesaidia kufanikisha ndani  ya Jamhuri ya Sudan Kusini.