UN

Lazima juhudi zaidi zichukuliwe kunusuru bayo-anuai:UN

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bayo-anuai unaendelea mjini Sharm El-Sheikh nchini Misri kujadili mbinu za kunusuru bayo-anuai ambayo inazidi kutoweka duniani.

UN yahaha machafuko yanaendelea Gaza

Wakati machafuko yakiendelea kushika kasi upya kwenye Ukanda wa Gaza , Umoja wa Mataifa unasema unafuatilia haki kwa karibu huku mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda huo Nickolay Mladenov akishirikiana na pande zote kujaribu kurejesha utulivu.

Sauti -
7'32"

Mara nyingi haki za watu wengi hubinywa kutokana na sababu kama vile, vita, mfumo wa utawala na hata mgawanyiko katika jamii.

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Ibara ya 6 inasema kila mtu anayo haki, binafsi au kwa ushirikiano na wengine, kuanzisha na kujadili dhana na kanuni mpya za haki za binadamu na kuzitetea ili zikubalike.” Lakini mara nyingi watu hawapati fursa ya kufanya hi

Sauti -
4'31"

Hali ya kibinadamu Batangafo, CAR si shwari

Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, umelaani janga la kibinadamu linaloendelea kwenye eneo la Batangafo mkoani Ouham kaskazini-maghaibi mwa nchi hiyo.

Vitisho vya Burundi dhidi ya tume ya uchunguzi ya UN havistahili na vifutwe:Bachelet

"Taarifa ya jana ya Balozi wa Burundi kwenye Umoja wa Mataifa Albert Shingiro kushambulia ripoti ya tume huru ya kimataifa ya Uchunguzi iliyoanzishwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa inasikitisha na kwa mada na sauti iliyotumika."

Siku ya UN, Guterres asema changamoto ni nyingi "lakini katu hatukati tamaa"

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni maadhimisho yanayolenga kusherehekea kuanza kutumika kwa katiba ya chombo hicho tarehe 24 Oktoba mwaka 1945.

UN na AU wajadili utekelezaji wa NEPAD

UN na AU wajadili utekelezaji wa NEPAD

Sauti -
1'43"

19 Oktoba 2018

UN na AU wajadili utekelezaji wa NEPAD. WFP yasaka suluhu ya uhaba wa chakula na utapiamlo nchini Uganda. Mashirika ya UN yaendelea kutoa msaada kwa manusura wa tetemeko Indonesia.

Sauti -
9'54"

Tusipofanikiwa Afrika, hatutafanikiwa popote pale- Bi. Espinosa

Mijadala kuhusu Afrika ikitamatishwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, hii leo Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wamefanya mjadala wa wazi kuhusu utekelezaji wa ubia mpya wa maendeleo barani Afrika, NEPAD sambamba na ushirikiano wa kimataifa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

Uganda imesema mkutano kati ya UN na AU ni ishara ya kupewa kipaumbele mawazo ya Afrika.

Mkutano wa AU na UN ukielekea ukingoni mjini New York, Uganda yasema ni ishara ya kupatiwa kipaumbele mawazo ya  bara la Afrika. 

Sauti -
1'29"