UN

Vitisho vya Burundi dhidi ya tume ya uchunguzi ya UN havistahili na vifutwe:Bachelet

"Taarifa ya jana ya Balozi wa Burundi kwenye Umoja wa Mataifa Albert Shingiro kushambulia ripoti ya tume huru ya kimataifa ya Uchunguzi iliyoanzishwa na Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa inasikitisha na kwa mada na sauti iliyotumika."

Siku ya UN, Guterres asema changamoto ni nyingi "lakini katu hatukati tamaa"

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni maadhimisho yanayolenga kusherehekea kuanza kutumika kwa katiba ya chombo hicho tarehe 24 Oktoba mwaka 1945.

UN na AU wajadili utekelezaji wa NEPAD

UN na AU wajadili utekelezaji wa NEPAD

Sauti -
1'43"

19 Oktoba 2018

UN na AU wajadili utekelezaji wa NEPAD. WFP yasaka suluhu ya uhaba wa chakula na utapiamlo nchini Uganda. Mashirika ya UN yaendelea kutoa msaada kwa manusura wa tetemeko Indonesia.

Sauti -
9'54"

Tusipofanikiwa Afrika, hatutafanikiwa popote pale- Bi. Espinosa

Mijadala kuhusu Afrika ikitamatishwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, hii leo Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wamefanya mjadala wa wazi kuhusu utekelezaji wa ubia mpya wa maendeleo barani Afrika, NEPAD sambamba na ushirikiano wa kimataifa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

Uganda imesema mkutano kati ya UN na AU ni ishara ya kupewa kipaumbele mawazo ya Afrika.

Mkutano wa AU na UN ukielekea ukingoni mjini New York, Uganda yasema ni ishara ya kupatiwa kipaumbele mawazo ya  bara la Afrika. 

Sauti -
1'29"

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa yaorodhesha mateso wanayofanyiwa watu wa kawaida Equatoria Magharibu Sudan Kusini

Ripoti mpya ya UN  yaorodhesha mateso kwa raia wa kawaida nchini Sudan Kusini. 

Sauti -
2'8"

18 Oktoba 2018

Kamishina mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet awaambia SPLA-IO(RM) waachilieni huru wananchi mnaowashikilia mateka. Uganda yafurahishwa na mkutano wa AU na UN, yasema ni ishara ya kupatiwa kipaumbele mawazo ya bara la Afrika.

Sauti -
9'38"

Mkutano wa AU na UN ni ishara ya kupatiwa kipaumbele bara la Afrika

Mkutano wa kuimarisha  ubia kati ya Umoja wa Mataifa, UN na Muungano wa Afrika, AU ukitamatishwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Uganda imesema fursa hii ni ishara ya kuendelea kupatia umuhimu mawazo ya Afrika katika chombo hicho chenye wanachama 193.

UN na AU wazingatie vipaumbele ili kufikia malengo tuliyojiwekea- Guterres

Umoja wa Mataifa umesema bado una imani na uongozi wa Afrika katika kutatua matatizo ya bara hilo na kwamba Umoja wa Mataifa una nia ya dhati kutumia fursa zilizopo sasa kufanya kazi kwa karibu zaidi na Muungano wa Afrika, AU.