Skip to main content

Chuja:

UN Charter

UN Photo/Amanda Voisard

Guterres: Mwongozo wa kutatua changamoto za duniani ni katiba ya UN

Katiba ya Umoja wa Mataifa ikiwa inaelekea kutimiza miaka 75 juma hili Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterrres amesema changamoto lukuki zinazoikabili dunia hivi sasa zinahitaji mwongozo ili kuzitatua na mwongozo huo ni katikaba ya Umoja wa Mataifa.

Guterres kupitia ujumbe maalum wa maadhimisho ya miaka 75 ya katiba hiyo amesema leo hii dunia inakabiliwa na majanga , na kote duniani watu wanapaza sauti zao dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Sauti
2'8"

24 JUNI 2020

Katika Jarida la Umoja wa Matafa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameiasa dunia kufuata katiba ya Umoja wa Mataifa inayotimiza miaka 75 wiki hii katika kutatua changamoto za dunia ikiwemo janga la COVID-19

-Nchini Tanzania hospitali ya CCBRT ambayo ina asilimia 6 ya wahudumu wake wenye ulemavu imesema inachukua hatua zote kuwalinda dhidi ya COVID-19 na kutaka serikali kuweka miundombinu ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wakati wa janga la COVID-19

Sauti
12'43"