Umoja wa Mataifa

Wataalam wa UN wakaribisha uamuzi wa mahakama Guatemala

Uamuzi wa mahakama nchini Guatemala kuwa watu wa jamii ya asili ya Lxul Mayans niwaathirika wa mauaji ya kimbari pamoja na mauaji dhidi ya binadamu, ni tukio la kihistoria  ambalo linatoa mfano bora wa juhudi za kusaka haki siyo tu nchini humo pekee bali pia kikanda na kimataifa.

Shukran Nikki Haley kwa ushirikiano mzuri UN- Guterres

Msemaji wa Umoja wa Mataifa leo amethibitisha taarifa za kuachia ngazi kwa Mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Nikki Haley ambapo Katibu Mkuu Antonio Guterres amemshukuru kwa kazi na ushirikiano mzuri.

Dunia ijifunze kusamehe kama alivyofanya Mandela- Balozi Mero

Leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanapitisha azimio la kumuenzi aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela.

Kifo cha Annan kimewashtua wengi

Kufuatia  kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Saba wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa pamoja na watu waliowahi kufanya naye kazi wameendelea kutoa salamu zao za rambirambi kwa kiongozi huyo aliyeelezwa kuwa ni bingwa wa utu wa kibinadamu. 

Sauti -
1'55"

Haki za watoto ni haki za binadamu lazima ziheshimiwe:UNICEF

Haki za watoto ni haki za binadamu na zinapaswa kuheshimiwa na kutekelezwa katika kila ngazi kuanzia kwenye familia, jamii na hata serikali kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto

Sauti -
4'47"

Idadi kubwa ya wajane duniani ni mafukara

Katika kuadhimisha siku ya wajane duniani hii leo, Umoja wa Mataifa unasema idadi kubwa ya kundi hilo ni mafukara.

Manyanyaso na ukatili dhidi ya wazee vikome

Leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ukatili wanaofanyiwa wazee.

Mpango wa serikali walenga kukabiliana na umaskini Uganda

Licha ya kwamba umaskini katika dunia umetokomezwa kwa nusu tangu 2000, juhudi madhubuti zinahitajika ili kuimarisha mapato ya watu, kuondoa mateso na kujenga mbinu za kustahimili umaskini uliokithiri hususan katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. 

Sauti -
3'31"

Ulemavu hautuzuii kubadili maisha yetu

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakimbizi kutoka Burundi ambao waliamini kuwa maisha yao yatazidi kuwa duni kutokana na ulemavu, sasa nuru imeanza kuwaangazia baada ya kutumia stadi na maarifa yao kuboresha maisha. 

Sauti -
1'42"

Usawa wa kijinsia ndio mkatakati wangu-Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa uongozi wake unatilia mkazo usawa wa kijinsia katika ngazi zote husasan za Umoja wa Mataifa.

Sauti -
1'30"