Chuja:

ulemavu wa ngozi

UN News/Video capture

Serikali ya Tanzania itakomboa watu wenye ulemavu kwa kuboresha mfumo wa ajira serikalini -  Shega Mboya

Serikali nchini Tanzania imeshauriwa kuboresha Sekretarieti ya mfumo wa uombaji ajira kwa njia ya mtandao maarufu kama Ajira Portal ili uweze kuwatambua watu wenye ulemavu na hivyo kumiza matakwa ya sera ya ajira ambayo ina kipengele mahususi kinacholenga kuwajumuisha watu wenye ulemavu.  Ushauri huo umetolewa na Shega Mboya wa Morogoro, Tanzania ambaye pamoja na kuwa na elimu ya juu ya digrii mbili, hajaweza kupata ajira ingawa anaamini pamoja na vigezo vingine ambavyo anaamini anavyo, laiti mfumo wa kidijitali ungeweza kutambua watu wenye ulemavu, ingekuwa rahisi kwake na kwa wengine. Ham

Sauti
2'40"
UN /Marie Frechon

Ingawa kuna changamoto angalau Kenya imechukua hatua kutulinda watu wenye ulemavu wa ngozi- Mbunge Mwaura

Tarehe 13 mwezi Juni ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha jamii kuhusu haki za watu wenye ulemavu wa ngozi. Siku hii inaadhimishwa kwa kuzingatia changamoto wanazokabiliana nazo kundi hilo ikiwemo kutengwa, kunyanyapaliwa na pia hata kuuawa kwa fikra potofu ya kwamba viungo vyao vinaweza kutumika kwa ajili ya utajiri.

Nchini Kenya, moja ya mataifa ambayo kundi hilo limekumbwa na changamoto, tayari kuna watetezi ndani ya kundi hilo na miongoni mwao ni Isaac Mwaura, mlemavu wa ngozi ambaye ni wa kwanza kuchaguliwa kuwa mbunge kwenye bunge la Kenya.

Sauti
3'31"