Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo, Pramila Patten amepongeza uamuzi wa hivi karibuni wa Muungano wa Afrika, AU, wa kutenga mkutano mmoja kila mwaka kujadili kwa uwazi janga la ukatili wa kingono katika mizozo barani humo.