Hii leo katika kuadhimisha miaka 10 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia ukatili wa kingono kwenye mizozo, manusura wa ukatili huo wametoa shuhuda dhahiri za yale waliyopitia huku wakitaka hatua thabiti za usaidizi na uwajibishwaji wa waliowatendea makosa.