Maelfu ya watu nchini Somalia wamelazimika kukimbia makwao tangu mwezi Novemba mwaka jana kwa sababu ya uhaba mkubwa wa maji huku utabiri wa sasa ukionesha kwamba msimu wa mvua unaoanza Machi hadi Juni hautakuwa na mvua za kutosha, imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya binadamu na misaada ya dharura OCHA .
Baada ya kughubikwa na vita kwa zaidi ya miongo mitatu sasa, ukame wa hivi karibuni umezidisha adha kwa mamilioni ya Wasomali ambao sasa wanahitaji huduma za msingi kama maji, malazi, huduma za afya na chakula.
Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamezindua ombi la kukabiliana na ukame la dola milioni 710 kwa ajili ya msaada wa dharura kwa ajili ya kuwasaidia watu milioni 4.5 wanaothriwa na ukame nchini Somalia kwa ajili ya kipindi kuanzia sasa hadi mwezi Disemba.
Ukame mkubwa unaoshuhudiwa nchini Somalia huenda ukasababisha njaa kwa watu milioni 2.2 ikiwa ni takriban asilimia 18 ya watu nchini humo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba limeonya leo shirika la chakula na kilimo duniani, FAO.
Kuchukua tahadhari za mapema katika nchi zinazotabiriwa kukumbwa na majanga ya asili kunaweza kuzuia tishio la kutokea zahma ya kibinadamu au kunaweza kudhibiti athari kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la chakula na kilimo duniani , FAO.
Ripoti kutoka shirika la chakula na kilimo duniani FAO, imesema ongezeko la joto na ukosefu wa nvua kusini mwa bara la Afrika vitaathiri sana sekta ya kilimo mwaka huu, na kufanya usalishajji wa mazao kupungua kwa kiasi kikubwa.