Leo ni siku ya milima duniani. Umoja wa Mataifa unapigia chepuo maeneo hayo kwa kaulimbinu milima ni muhimu. Biashara mtandaoni ikiwezeshwa yaweza kuliinua bara la Afrika yasema UNCTAD, Mradi wa Benki ya Dunia Niger wakomesha hamahama ya wananchi kutokana na ukame.
Ongezeko la uelewa wa wananchi kuhusu rasilimali zilizopo na huduma wanazopata kutoka kwenye serikali zao ni moja ya mambo yaliyotajwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuwa yanasababisha wananchi kukosa imani na taasisi zao zinazowaongoza.