uhamiaji

Uhamiaji uwe ajenda ya kisiasa barani Afrika

Mkutano wa siku mbili kuhusu uhamiaji barani Afrika umekunja jamvi huko Geneva, Uswisi ambapo washiriki wametaka viongozi wa bara hilo wahamasishwe ili uhamiaji iwe ajenda ya kisiasa kwa nchi zao.

Makabila Kenya sasa ni 44, ni baada ya wamakonde na wahindi nao kutambuliwa

Uhamiaji kwa sasa unakumbwa na madhila makubwa. Watu wanahama kwa sababu mbalimbali ikiwemo kusaka maisha bora, elimu, ajira, kuanzisha familia na nyingine nyingi. Nchini Kenya wahamiaji walitoka mbali hata bara hindi na nchi jirani kama vile Tanzania na Msumbiji. 

Sauti -
4'2"

Uhamiaji umebisha hodi katika kila familia

Je wangapi kati yetu ndani ya familia zetu tuna historia ya uhamiaji zinazoimarisha urithi wa tamaduni zetu?

Ni swali la Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed wakati akifungua mkutano wa 51 wa kamisheni ya idadi ya watu na maendeleo hii leo jijini New York, Marekani.

Sauti -
1'25"

Wahamiaji watarajie nini kutoka Brussels?

 Viongozi waandamizi wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM pamoja na Muungano wa Ulaya, wakiwa Brussels Ubelgiji, wanajadili mustakhbali wa uhamiaji wakati huu ambapo kundi hilo linakabiliwa na sintofahamu.

Sauti -
1'20"

Sualala uhamiaji si la mtu mmoja:UM

Suala la uhamiaji ni mtambuka na sio la kushughulikiwa na mtu mmoja au taifa moja, linahitaji mshikanao wa kimataifa kulipatia ufumbuzi. 

Sauti -
1'37"

26 Machi 2016

Jaridani leo tunaangazia swala la uhamiaji na mchango wa radio za kijamii katika kumuendeleza mwanamke wa kijijini. Tunamulika pia ujumbe wa vijana wanaoshiriki mkutano wa kuchukua hatua za kimataifa ili  kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs huko Bonn nchini Ujerumani. 

Sauti -
11'2"

Uhamiaji ni suala mtambuka, wabunge walivalia njuga: UN

Wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani wanakutana makao makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini New York Marekani kubadilisha mawazo ya jinsi ya kukabiliana na suala mtambuka la uhamiaji.

Sauti -
1'40"

23 Februari 2018

Jaridani leo tunaanza na habari za kusikitisha ya wakimbizi kuuawa nchini Rwnada na wengine kujeruhiwa. Tunaangazia pia mkutano wa wajumbe unaondelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakijadili suala mtambuka la uhamiaji.

Sauti -
11'7"

Uhamiaji ni suala mtambuka, wabunge walivalia njua: UN

Wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani wanakutana makao makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini New York Marekani kubadilisha mawazo ya jinsi ya kukabiliana na suala mtambuka la uhamiaji.  

Katu hatutokubali utumwa urejee Afrika- Guterres

Mkutano wa kawaida wa 30 wa viongozi wa Afrika ukiendelea huko Addis Ababa, Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja mambo matano ya kuimarisha ushirikiano kati a pande mbili hizo.

Sauti -