uhamiaji

Nilikuwa na hofu ugenini, lakini sera za Rwanda zimeniondoa uhofu- Mhamiaji

Mpango wa kujumuisha wakimbizi katika maendeleo ya kiuchumi kwenye mji mkuu wa Rwanda, Kigali, umechangia katika wakimbizi kuanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zimebuni ajira kwa watu 2,600 nchini humo, ikiwemo biashara ya kuuza mitungi ya gesi inayomilikiwa na mkimbizi kutoka Burundi.

Sauti -
2'15"

28 Desemba 2018

Jaridani hii leo na Siraj Kalyango tunaanza na Sudan ambako  yaripotiwa maelfu ya watu wanaandamana kupinga ongezeko la bei za bidhaa sambamba na uhaba wa chakula na mafuta ya gari.

Sauti -
11'44"

Uhamiaji uzingatie utu

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhamiaji hii leo, Umoja wa Mataifa unasisitiza uhamiaji unaozingatia utu.

Sauti -
2'28"

Uhamiaji uwe wa utu kwa kila mtu- IOM

Katika kuadhimisha siku ya uhamiaji duniani hii leo, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, António Vitorino ametaka hatua zaidi na za dharura zichukuliwe ili kulinda kundi hilo ambalo kila uchwao linakumbwa na madhila kote ulimwenguni.

Mkataba wa uhamiaji wapitishwa rasmi

Baaa ya majadiliano ya miezi, wiki, siku na saa, hatimaye mkataba kwa kimataifa ambao ni wa kihistoria kuhusu wahamiaji leo umepitishwa Rasmi mjini Marrakesh Morocco. Grace Kaneita na taarifa kamili.

Sauti -
1'43"

Algeria acheni kufukuza wahamiaji na kuwatelekeza jangwani- Mtaalamu

Ukatili unaokumba wahamiaji watoto na watu wazima kutoka nchi za Afrika Magharibi unapaswa kushawishi jamii yenye utu duniani kuchukua hatua, amesema mtaalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Tuimarishe ushirikiano wa kimataifa ili kunusuru uhamiaji- Grandi

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ametoa wito kwa mataifa kushirikiana ili kupata ufumbuzi wa suala la wakimbizi akisema makubaliano mapya  kuhusu wakimbizi  yatageuza hifadhi kuwa jibu mujarabu.

Ukitaka kuhama tafuta viza hama kihalali- wimbo Fela wa Degg J

Uhamiaji ni suala ambalo linaibua hisia tofauti kwa jinsi linavyochukuliwa na watu tofauti. Wakati uhamiaji unatoa fursa na faida kwa wanaohama na wenyeji wanakofikia lakini kuna changamoto nyingi katika uhamiaji.

Sauti -
4'2"

25 Septemba 2018

Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza leo na Katibu Mkuu amesema ni dhahiri shairi dunia imeparaganyika. Hiyo ni miongoni tu mwa habari tulizo nazo hii leo zikiletwa kwenu na Siraj Kalyango.

Sauti -
12'57"