Kamati ya Umoja wa Mataifa ambayo inafutilia haki za watoto inazinduliwa rasmi leo Alhamisi ikiwa na malengo ya kusaidia nchi kutekekeza makubaliano yanayohusu kuuzwa kwa watoto, watoto kutumiwa katika umalaya na biashara ya picha za uchi za watoto.
Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameongeza sauti yake katika kulaani mashambulizi ya risasi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki nchini Marekani na kusisitiza kwamba sio Marekani tu bali mataifa yote yanapaswa kufanya juhudi zaidi kukomesha ubaguzi.