Nchini Uganda, baada ya janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 kukwamisha harakati za vijana ikiwemo wanamuziki kuendesha shughuli zao, kijana mmoja mwanamuziki ameamua kurejea katika kazi yake ya useremali ili aweze kutunza familia yake.
Sasa ni makala ambapo tunafuatilia hali ilivyo na mikakati inayowekwa na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi
Shirka la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Uganda limesikitishwa na kifo cha kwanza kabisa cha mkimbizi kutokana na virusi vya corona au COVID-19 tangu mlipuko wake utangazwe nchini humo mnamo Machi mwaka huu.
Katika juhudu za binafsi za kufikia lengo namba moja la malengo ya maendeleo endelevu au SDGs, mzee mmoja nchini Uganda ameamua kujikwamua kutoka katika lindi la umaskini kwa kujiimarisha katika kilimo cha pilipili.
Kutokana na mafuriko ya kila mwaka yanayoikumba wilaya ya Kasese nchini Uganda, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na serikali ya Uganda, wanaendelea kuimarisha mifumo ya kuhakikisha kunakuwa na mazingira ya kuchukua hatua za haraka kunapokuwa na dharura kama hizo.