UGANDA

25 Julai 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Arnold Kayanda anakuletea

Sauti -
11'39"

Uchafuzi wa Mto Kafu na athari zake wamulikwa, Uganda

Maeneo oevu ni sehemu muhimu katika suala zima la uhifadhi wa mazingira ambalo linapigiwa chepuo katika Malengo ya maendeleo endelevu (SDGS) hususani lengo namba 15, linalohimiza uhifadhi wa mazingira yakiwemo maeneo oevu  pamoja na matumizi endelevu ya misitu na kuzuia kuenea kwa hali ya jangwa.

Sauti -
4'30"

22 Julai 2019

Katika Jarida letu la Habari hii leo Arnold Kayanda anakuletea

-Mkurugenzi mkuu wa shirika la nguvu za atomiki duniani IAEA Yukiya Amano aaga dunia , rambirambi zaendelea kumiminika kutoka kila kona

Sauti -
14'28"

Msighafirike, saidieni DRC ili iondokane na changamoto zake- WHO

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema virusi vya Ebola ni miongoni mwa changamoto lukuki zinazokabili jamii za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwa hiyo jamii ya kimataifa kuendelea kuonyesha usaidizi na mshikamano na wananchi wa taifa hilo la Maziwa Makuu Afrika.

Vijana kukamatwa juu ya mkopo wa serikali, Uganda

Katika harakati za kuhakikisha kwamba vijana wanapata ajira sio tu kwa kuajiriwa lakini kwa pia kwa kujiajiri kupitia ubunifu wa biashara mbali mbali, serikali zimeanza kuchukua hatua na kuweka programmu ambazo zinatoa mikopo kwa vijana kwa mfano vikundi kwa ajili ya kufanya biashara.

Sauti -
4'9"

17 Julai 2019

Katika Jarifda la Habari hii leo assumpta Massoi anakuletea

- Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu tathimini ya malengo ya maendeleo endelevu linaendela kwenye Umoja wa Mataifa na sauti ya vijana vimetajwa kuwa muhimu kusongesha ajenda ya 2030

Sauti -
12'48"

Wanawake wataka nafasi katika vyombo vya habari ili kustawi, Uganda

Nafasi ya mwanamke iwe katika siasa, uchumi au masuala mengine ya kijamii ni muhimu sana sio tu kwa kumuinua na kumuwezesha mwanamke lakini pia katika kuendeleza jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Sauti -
3'58"

16 Julai 2019

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Jukwaa la ngazi ya juu la ngazi ya mawaziri kuhusu tathimini ya SDGs na UN inasema bila usawa na ujumuishi ni mtihani kufikia malengo hayo

Sauti -
12'27"

Korea yatoa tani 5,000 za chakula kwa wakimbizi, Uganda

Shrika la Mpango wa chakula duniani (WFP) nchini Uganda limekaribisha mchango tani 5,000 za mchele kutoka kwa seriakli ya Korea Kusini amabyo imeitikia mahitaji ya cahkula yanayongezeka kila uchao miongoni mwa wakimbizi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. 

Chumia juani ujanani ili ulie kivulini uzeeni (Sehemu ya pili)

Ule usemi wa wahenga ya kwamba mchumia juani  hulia kivulini ni suala ambalo linaonekana kuwa na mashiko iwapo litapatiwa mtazamo mpana zaidi na kuhusishwa na maisha ya sasa na baadaye.

Sauti -
4'3"