UGANDA

Wahudumu wa afya na serikali Uganda wanafanya kazi nzuri kudhibiti Ebola:WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limewapongeza wahudumu wa afya na wizara ya afya ya Uganda kwa hatua za haraka na maandalizi ya kupambana na mlipuko wa Ebola uliozuka hivi karibuni nchini humo. 

Mabadiliko ya tabianchi ni janga kwa wafugaji Uganda

Mabadiliko ya tabianchi ni janga ambalo linaikabili dunia hii leo ambapo Umoja wa Mataifa na washirika wake kupitia lengo nambari 13 la ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endeleve au SDGs, wamekuwa msatari wa mbele kubonga bongo ili  kutafuta suluhisho ikiwa ni pamoja na  kuhamisha serikali na asa

Sauti -
3'48"

27 Juni 2019

Miongoni mwa habari anazokuletea hii leo arnold Kayanda katika Jarida laletu ni pamoja na 

-Halahala yatolewa na shirika la afya ulimwenguni watu kupata chanjo ya surua kabla ya kwenda nchi zenye mlipuko wa ugonjwa huo

Sauti -
12'43"

Vituo vya wakimbizi vyazidiwa Uganda maelfu wakiendelea kumiminika toka DRC:UNHCR

Mapigano mapya Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC yamewafurusha watu takribani 7500 na kuwalazimisha kukimbilia nchi jirani ya Uganda tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Juni na kuongeza shinikizo katika vituo vya wakimbizi ambavyo tayari vilikuwa vimezidiwa uwezo limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Usaidizi kwa wakimbizi uende sanjari na kusaidia wenyeji- Uganda

Idadi ya wakimbizi wanaomiminika Uganda ikiripotiwa kila uchao, serikali ya Uganda imesema mkakati wa manufaa zaidi wa kuweza kusaidia kundi hilo ni lazima uweze kuwa na manufaa pia kwa wenyeji ambao kwa mujibu wa mfumo wa taifa hilo wanatangamana na wakimbizi.  Arnold Kayanda na  maelezo zaidi.

Sauti -
2'16"

Kuwasaidia wakimbizi na wenyeji wao, ni njia nzuri ya kuwahudumia watu waliotawanywa-Uganda

Idadi ya wakimbizi wanaomiminika Uganda ikiripotiwa kila uchao, serikali ya Uganda imesema mkakati wa manufaa zaidi wa kuweza kusaidia kundi hilo ni lazima uweze kuwa na manufaa pia kwa wenyeji ambao kwa mujibu wa mfumo wa taifa hilo wanatangamana na wakimizi. 

Mwanafunzi mkimbizi wa DRC atunukiwa tuzo Uganda

Mamilioni ya watu wameendelea kufungasha virago kila uchao kwenda kusaka usalama wakikimbia vita, mateso, mauaji, njaa na sambabu zingine mbalimbali. Japo wakimbizi hawa wanaonekana mzingo machoni mwa wengi Umoja wa Mataifa unasema dunia ikiwakumbatia itaoona mchango wao na faida yao.

Sauti -
4'7"

20 Juni 2019

Je wajua kuwa vita na mizozo husababisha kiwewe kwa watoto na kuwafanya washindwe kujifunza hata wakiwa ugenini?

Sauti -
11'48"

FAO nayo mstari wa mbele kuepusha mizozano kati ya wenyeji na wakimbizi

Wakati takwimu mpya za Umoja wa Mataifa zikionesha kuwa idadi ya wakimbizi duniani ikiwa ni zaidi ya milioni 70.8, shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limetaja hatua inazochukua kuepusha mvutano kati ya wakimbizi na wenyeji wao iwe ndani ya nchi zao au ugenini.
 

Wananchi Uganda wazungumzia harakati dhidi ya Ebola

Mamlaka za wilaya mbalimbali za mpakani kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), zimeimarisha juhudi za uhamasishaji wa jamii kuhusu tishio kufuatia mlipuko wa Ebola na njia za kinga baada ya watu watatu kufariki dunia na wengine 10 waliokutana na marehemu hao wakiendelea kufanyi

Sauti -
2'48"