UGANDA

16 Machi 2018

Katika jarida la leo tunaangazia wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wanaoingia Uganda.  Tunaangazia pia usawa wa kijinsia, jambo ambalo linajadiliwa kwenye mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake duninai, CSW62, unaoendelea  jijini New York, Marekani. Sikiliza pia makala ikiangazia jinsi muziki umebadili mtazamo wa wakimbizi wa CAR na neno la wiki.   

Sauti -
9'59"

Bidhaa za tumbaku lazima zidhibitiwe

Bidhaa za tumbaku zinasababisha madhara mengi sana hususani kiafya. Shirika la afya duniani WHO sasa linataka kila nchi mwanachaka kuchukua hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo kwa kuweka sheria na kuzitekeleza.

09 Machi 2018

Katika jarida la leo tunaanza na mwuongozo mpya uliyotolewa na WHO kuhusu jukumu la sheria dhidi ya bidhaa za tumbaku. Tunaangazia pia jinsi Tanzania imejipanga kufanikisha maendeleo ya uchumi kutokana na viwanda. Pata pia makala ya midundo na uchambuzi wa neno la wiki. 

Sauti -
11'27"

UNAIDS yashuhudia jinsi ufalme wa Bunyoro unavyokabiliana na UKIMWI

Ufalme wa Bunyoro umepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya ukimwi , lakini pia umejinyakulia sifa kemkem kutoka kwa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS, Bwana Michel Sidibe ambaye yuko ziarani nchini Uganda, kwa kudumisha utu wa kuwapokea wakimbizi lukuki wengi kutoka Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Sauti -
1'44"

Heko Bunyoro kwa kupambana na UKIMWI-UNAIDS

Mfalme Iguru wa Pili, wa Bunyoro Kitara nchini Uganda  anasifika sana kwa kitendo chake cha kila wakati kutumia hotuba zake kuhamasisha watu wake kujikinga dhidi ya UKIMWI na hii imezaa matunda hadi kupatiwa pongezi na Umoja wa Mataifa.

02 Machi 2018

Katika jarida la leo tunaanza na usawa wa kijinsia katika siasa. Tunamulika pia changamoto zinazowakumba wakimbizi waRohingya ikiwemo hofu ya kushambuliwa na tembo. Jifunze pia neno la wiki ambako tunaangazi neno "Kimanda".

Sauti -
9'58"