UGANDA

Wanaharakati wakemea wanawake kuvuliwa nguo hadharani Uganda

Ukatili wa kijinsia ni jambo linaloleta hofu kubwa kwa jamii hususan wanawake na watoto wa kike. Ukatili huo ni wa aina mbalimbali ikiwemo wa kingono, kipigo na hata manyanyaso.

Sauti -
3'31"

27 Februari 2018

Katika jarida la leo tunaanza na hali ya wakimbizi nchini Uganda. Pia tunaangazia mlipuko wa Homa ya Lassa nchini Nigeria, na je, Syria kulikoni baada ya sitisho la mapigano kupitiswa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumamosi wiki jana? 

Sauti -
10'41"

26 Februari 2018

Haki za binadamu pamoja na tatizo la njaa Sudan Kusini ni baadhi ya habari zilizopo katika jarida la leo. Pia tunakuletea makala ya tabianchi ikiangazia kongamano la watu wa asili kutoka  eneo la maziwa makuu  barani Afrika.

Sauti -
9'57"

Tunasaka misaada endelevu badala ya dharura pekee- UNHCR

Wakimbizi wanapowasili ugenini huduma ya kwanza ni mahitaji ya dharura kama vile maji, huduma  za afya na malazi kinachofuatia ni huduma za baadaye na endelevu. Mahitaji kama vile stadi za kazi na hata ajira.

Wakimbizi Kyaka II, Uganda walilia huduma za afya

Nchini Uganda wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wahisani wametembelea kituo cha hifadhi ya wakimbizi cha Kyaka II ili kutathmini mahitaji ya kituo hicho na wenyeji wanaokizunguka.

Kipindupindu chalipuka kambi ya wakimbizi kyangwali, 400 walazwa

Wakati mamia ya wanaokimbia mzoozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiendelea kumiminika nchini Uganda , wakimbizi sita wamethibitishwa kuaga dunia huku wengine zaidi ya 400, wakilazwa hospitalini baada ya kuugua ugonjwa unaoshukiwa kuwa kipindupindu katika kambi ya Kyangwali nchini Uganda. 

Sauti -
1'21"

Maiti za ndugu zetu zimetapakaa Ituri

Raia wanaokimbia mapigano ya  kikabila kwenye jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wameelezea madhila wanayokumbana nayo baada ya safari ndefu na ya  hatari ya kuingia Uganda kupitia ziwa Albert.

Sauti -
1'56"

Wanamazingira Afrika mashariki wanolewa Bujumbura

Katika jitihada za kuchagiza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka waka 2030, Umoja wa Mataifa na washirika wake wameendeleza kampeni mbalimbali duniani kuhimiza serikali na asasi za kiraia kuelemisha jamii katika utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Sauti -
4'10"

Malefu wanendelea kufungasha virago Ituri DRC na kumiminika Uganda

Shirika la Umoja w aMataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limeripoti kuwa wakimbizi takribani 4,000 wamekimbilia Uganda kufuatia kush

Sauti -
1'5"

Maelfu wanaendelea kufungasha virago Ituri, DRC na kumiminika Uganda

Shirika la Umoja w aMataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limeripoti kuwa wakimbizi takribani 4,000 wamekimbilia Uganda kufuatia kushamiri kwa mzozo wa kikabila Jimbo la Ituri na mashambulizi ya vikundi vilivyojihami Jimboni Kivu Kaskazini katika kipindi cha wiki moja tu.