Nchini Uganda, wakimbizi wanaoishi kwenye makazi ya Kyaka na Kyangwali pamoja na wenyeji wao wameanza kunufaika na miradi miwili ya maji iliyojengwa na shirika la uhamiaji duniani, IOM kwa msaada wa fedha kutoka Muungano wa Ulaya, EU.
Katika kuitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadih kupata elimu, nchini Uganda, serikali ya Japani imekamilisha ujenzi wa maabara ya sayansi kwenye shule ya secondari ya Kyangwali katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali na kuikabidhi kwa jamii husika. John Kibego na maelezo Zaidi.
Kutana na Anita na Janet wasichana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambao wote wana umri wa miaka 13 na wanaishi katika makazi ya wakimbzi ya Kyaka nchini Uganda marafiki na wanasaidiana. Jason Nyakundi na taarifa zaidi
Wahenga walisema siri ya mtungi aijuaye kata na uchungu wa ajira ya mtoto anaujua mtoto aliyeipitia, kauli hiyo imetolewa na Molly Namirembe mwanaharakati wa kupambana na ajira ya watoto nchini Uganda ambaye yeye mwenyewe alipitia madhila hayo na jinamizi lake linamtesa hadi sasa. Kupitia mradi wa SCREAM unaosaidiwa na shirika la kazi duniani ILO Namirembe amedhamiria kupambana na ajira hiyo nchini mwake.
Leo Oktoba Mosi ni siku ya wazee duniani ambapo mwaka huu kauli mbiu ni “safari ya kuzeeka kwa usawa” kwa kutambua kwamba malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yatafikiwa pale tu watu wa umri wote wamejumuishwa.
Wakati viongozi wa dunia wamepitisha azimio la kisiasa la kuhakikisha huduma ya afya kwa wote inapatikana kwa kila mkazi wa dunia ifikapo mwaka 2030, nchini Uganda mwandishi wetu John Kibego amevinjari katika maeneo ya Hoima ili kuweza kupata maoni ya wananchi kuhusu huduma hiyo adhimu.
Maelfu ya watu hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kutopata tahadhari ya mapema ya majanga yatokanayo na hali ya hewa kama vimbunga, mafuriko, na hata matetemeko ya ardhi. Ili kuokoa maisha shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO sasa linachukua hatua likishirikiana na nchi mbalimbali kuhakikisha tahadhari inachukuliwa mapema.
Nchini Uganda mtangazaji wa kipindi cha masuala ya kijamii mjini Hoima ameleta nuru kwa watoto wengi waliohatarini baada ya kuanzisha kituo cha kulea watoto wakiwemo yatima na wanaozaliwa na watu wenye matatizo ya akili. Je, mwanahabari huyo amegeukaje kuwa mhudumu wa kibinadamu?
Hali ya kuwa mkimbizi kwa sababu yoyote ile ni changamoto kubwa hasa kwa kutojua mustakabali wako na endapo ulikoikimbia kutatengamaa. Mkimbizi Jenipher Mutamba toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Oruchinga nchini Uganda anasema wakati mwingine ukimbizi hufungua mlango wa baraka katika maisha. John Kibego na taarifa zaidi
Uganda ni moja ya nchi zilizo na idadi kubwa ya watu na idadi hiyo inaongezeka kila uchao. Kwa sasa nchi hiyo ina takriban watu milioni 40 na zaidi ya asilimia 75 wanaishi vijijini na asilimia 80 ya watu hao wako katika mashamba ya kurithi ambayo mengi hazijaandikishwa, kupimwa wala kuingizwa katika ramani.