UGANDA

Uganda nayo yaanza kutoa chanjo dhidi ya COVID-19

Nchini Uganda kazi ya kuwapatia chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 wafanyakazi walio mstari wa mbele wakiwemo wahudumu wa afya imeanza kufuatia taifa hilo la Afrika Mashariki kupokea shehena ya chanjo kutoka COVAX ambao ni mfumo wa kimataifa wa kusaka na kusambaza chanjo za COVID-19.

Ingawa Corona ilininyima masomo na kunipora miguu yangu, haitopokonya ndoto yangu: mtoto Chirstine 

Kutana na binti kutoka Uganda, Christine Joyce ambaye anasema asilani hatolisahau janga la corona au COVID-19 ambalo mbali ya kumnyima masomo wakati wa sheria za kusalia majumbani limechangia kumwacha na kilema cha maisha. Hata hivyo amesema hatokata tamaa ya kutimiza ndoto yake ya kuendelea na masomo na hatimaye siku moja kuwa daktari.

UNICEF yapokea vifaa kusaidia afya ya mama na mtoto nchini Uganda 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mapema mwezi huu limepokea shehena ya vifaa tiba mbalimbali vya kusaidia afya ya mama na mtoto nchini Uganda. Taarifa ya mwandishi wetu wa Uganda.

Usiombe ukutwe na hali ya kukosa utaifa!  

Kutana na Mpho Modise, mama wa watoto wanne ambaye licha ya kuishi nchini Afrika Kusini hana uhakika wa utaifa wake na hivyo anashindwa kupata huduma za msingi kama vile afya na hofu yake kubwa ni kwamba shida inayomkabili yeye ya kukosa utaifa inaweza kuhamia kwa watoto wake labda apate utaifa wa Afrika Kusini.

Mume wangu na wanangu 4 waliuawa napata faraja kwa kuwasaidia wanawake wengine:Sabuni Chikunda

Tukiwa bado na siku 16 za harakati za kupinga uakatili wa kijinsia dhidi ya wanawake, leo tunamulika mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , Francoise Sabuni Chikunda ambaye amepitia madhila yasiyoelezeka, ikiwemo kubakwa na hata familia yake kuuawa, lakini yote hayo hayakumkatisha tamaa bali yamempa ujasiri wa kuwa nuru ya wanawake wakimbizi wenzake katika makazi ya wakimbizi ya Nakivale nchini Uganda.

COVID-19 yamlazimisha mwalimu kusaka kipato mbadala nchini Uganda

Leo ikiwa ni siku ya walimu duniani, ambayo mwaka huu inaadhimishwa kukiwa na changamoto kubwa kwa walimu na wanafunzi kufuatia janga la corona au COVID-19, huku Umoja wa Mataifa ukisema takriban wanafunzi bilioni 1.6 ambao ni zaidi ya wanafunzi wote duniani waliojiandikisha shule wameathiriwa na kufungwa kwa shule. 

UNHCR kuendeleza huduma licha wadau wake wa kibinadamu kufungiwa Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifala Kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Uganda limesema linajitahidi kuhakikisha kwamba hatua ya serilkali ya kuyasimamisha mashirika ya misaada yasiyo ya kiserikali 208 nchini humo kwa kutokidhi vigezo vya sheria kuhudumia wakimbizi , haiathiri utoaji wa huduma kwa wakimbizi hao.

Wazazi na wanafunzi washika hatamu kwenye masomo Uganda wakati huu wa Corona

Gonjwa wa Corona au COVID-19 likiendelea kusababisha baadhi ya nchi kufunga shule na vyuo na hivyo wanafunzi kulazimika kusomea majumbani, walimu, wazazi na wanafunzi nchini Uganda, wamezungumzia changamoto wanazokumbana  nazo.

Ubia wa UNICEF na serikali Uganda waleta nuru kwa waishio na VVU 

Nchini Uganda, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kwa kushirikiana na serikali, limechukua hatua kuhakikisha kuwa huduma za msingi za kiafya za kuokoa maisha ikiwemo dawa za kupunguza makali ya UKIMWI zinapatikana hata wakati huu wa vizuizi vya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. 

Kutoka uimbaji jukwaani hadi kuuza vijiko mitaani, kulikoni? COVID-19

Nchini Uganda, baada ya janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 kukwamisha harakati za vijana ikiwemo wanamuziki kuendesha shughuli zao, kijana mmoja mwanamuziki ameamua kurejea katika kazi yake ya useremali ili aweze kutunza familia yake.