Kutana na Solomon Kingi Benge mwanzilishi wa kituo cha mafunzo ya trknolojia ya roboti .Ameamua kuusambaza ujuzi wake kwa wanafunzi katika shule nchini Uganda.
Mradi wa maji safi na salama unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kwenye makazi ya wakimbizi ya Bidibidi nchini Uganda umekuwa faraja sio tu kwa wakimbizi bali pia jamii zinazowahifadhi.
Nchini Uganda, wakimbizi wanaoishi kwenye makazi ya Kyaka na Kyangwali pamoja na wenyeji wao wameanza kunufaika na miradi miwili ya maji iliyojengwa na shirika la uhamiaji duniani, IOM kwa msaada wa fedha kutoka Muungano wa Ulaya, EU.
Katika kuitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadih kupata elimu, nchini Uganda, serikali ya Japani imekamilisha ujenzi wa maabara ya sayansi kwenye shule ya secondari ya Kyangwali katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali na kuikabidhi kwa jamii husika. John Kibego na maelezo Zaidi.
Kutana na Anita na Janet wasichana wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambao wote wana umri wa miaka 13 na wanaishi katika makazi ya wakimbzi ya Kyaka nchini Uganda marafiki na wanasaidiana. Jason Nyakundi na taarifa zaidi
Wahenga walisema siri ya mtungi aijuaye kata na uchungu wa ajira ya mtoto anaujua mtoto aliyeipitia, kauli hiyo imetolewa na Molly Namirembe mwanaharakati wa kupambana na ajira ya watoto nchini Uganda ambaye yeye mwenyewe alipitia madhila hayo na jinamizi lake linamtesa hadi sasa. Kupitia mradi wa SCREAM unaosaidiwa na shirika la kazi duniani ILO Namirembe amedhamiria kupambana na ajira hiyo nchini mwake.
Leo Oktoba Mosi ni siku ya wazee duniani ambapo mwaka huu kauli mbiu ni “safari ya kuzeeka kwa usawa” kwa kutambua kwamba malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yatafikiwa pale tu watu wa umri wote wamejumuishwa.
Wakati viongozi wa dunia wamepitisha azimio la kisiasa la kuhakikisha huduma ya afya kwa wote inapatikana kwa kila mkazi wa dunia ifikapo mwaka 2030, nchini Uganda mwandishi wetu John Kibego amevinjari katika maeneo ya Hoima ili kuweza kupata maoni ya wananchi kuhusu huduma hiyo adhimu.
Maelfu ya watu hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kutopata tahadhari ya mapema ya majanga yatokanayo na hali ya hewa kama vimbunga, mafuriko, na hata matetemeko ya ardhi. Ili kuokoa maisha shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO sasa linachukua hatua likishirikiana na nchi mbalimbali kuhakikisha tahadhari inachukuliwa mapema.