Baada ya Sweden kupitia shirika lake la misaada ya maendeleo ya kimataifa, SIDA kuitikia wito wa usaidizi wa fedha wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, Unicef nchini Uganda, sasa kuna matumaini makubwa ya kwamba huduma za afya kwa wajawazito, barubaru na watoto wachanga zitaimarika.