Kufuatia kuungua kwa sehemu ya Kanisa Kuu Katoliki la kale, Notre Dame huko Paris nchini Ufaransa hapo jana, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeunda kikundi cha wataalamu kwa ajili ya tathmini ya haraka ya uharibifu itakayoanza mapema iwezekanavyo.