Udumavu

World Bank/Maria Fleischmann

Kutoa ni moyo si utajiri

Bi Neema Mustafa mkazi wa Kijiji cha Kiswanya, wilayani Kilombero, Morogoro Tanzania ni mtu mwenye ulemavu ambaye anaishi katika hali ya kupooza kwa zaidi ya miaka 20 tangu  alipopooza mwili wake akiwa na msichana mdogo wa umri wa takribani miaka 20. Neema aliamua kumsaidia mtoto Omar ambaye alikuwa katika hali mbaya ya utapiamlo uliosababisha udumavu baada ya changamoto za maisha ya wazazi wa mtoto huyo kuwafanya washindwe kumlea.

Sauti
4'15"
© UNICEF/Andrea Campeanu

UNICEF inasema COVID-19 imeongeza shida ya watoto wenye utapiamlo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema kuwa nyongeza ya watoto milioni 6.7 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaweza kupata tatizo la kuwa na uzito mdogo zaidi kulingana na urefu wao na hivyo kuwa na unyafuzi kutokana na madhara ya kiuchumi na kijamii yatokanayo na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.  Flora Nducha na taarifa zaidi.

Sauti
2'37"