UDHR70

Mfuko wa manusura wa utesaji ni mkombozi kwa manusura na familia zao

Ibara ya 5 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu wa 2018, inaweka bayana kuwa hakuna mtu yeyote anayepaswa kuteswa kwa sababu yoyote ile. 
 

Nchi zinatakiwa kubadili sheria zao ili kwenda sawa na mbinu za sasa za utumwa na utwana.

Ibara ya 4 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu wa 2018, inaeleza kinagaubaga kuwa hakuna mtu anayestahili kugeuzwa mtumwa na wala kuwa mtwana wa mtu yeyote.

Sauti -
2'51"

Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Kila mtu anastahili kuwa na haki zote na uhuru wote ambao umeelezwa katika tamko hili bila ubaguzi wa aina yoyote kama vile rangi, taifa, jinsia, lugha, dini, siasa, fikra, asili ya taifa la mtu, miliki , kuzailiwa au kwa hali nyingine yoyote.

Sauti -
52"