Uchumi

19 Aprili 2019

Mkutano hwa nne wa uchangishaji fedha kwa ajili ya maendeleo umefanyika juma hili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ukiwaleta pamoja wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mawaziri  wapatao 30 kutoka mataifa mbali mbali.

Sauti -
9'57"

Serikali zisipochukua hatua dhidi ya mifumo ya fedha kutimiza SDGs itakuwa ndoto:UN/IMF/WTO

Mashirika zaidi ya sita ya kimataifa yakiongozwa na Umoja wa Mataifa likiwemo shirika la fedha duniani IMF, Benki ya Dunia na shirika la biashara duniani WTO kwa pamoja wametoa tahadhari katika ripoti yao mpya wakionya kwamba mifumo ya fedha ya kitaifa na kimataifa isipofanyiwa marekebisho na kufufuliwa basi itakuwa ndoto kwa serikali duniani kutimiza ahadi ya masuala muhimu kama kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kutokomeza njaa ifikapo 2030.

Uchumi wa dunia wadorora, chonde chonde watunga sera msipeleke chombo mrama- IMF

Shirika la fedha duniani, IMF limesema uchumi wa dunia unasuasua na hivyo linataka viongozi duniani wawe makini katika kile wanachofanya.

Nchi za Afrika zapokea mitaji mingi isiyo rasmi kuliko ilivyodhaniwa- IMF

Ripoti mpya ya shirika la fedha duniani, IMF iliweka bayana juu ya ongezeko la mitaji huko Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara na hii leo mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo anaweka bayana kile kilichovutia wawekezaji.

Matumizi endelevu ya bahari yaangaziwa Nairobi

Mkutano wa kimataifa kuhusu matumizi endelevu ya bahari kwa ajili ya ukuaji wa uchumi ukiingia siku ya pili hii leo huko Nairobi, Kenya, mwakilishi wa serikali ya Zanzibar kutoka Tanzania amezungumzia umuhimu wa bahari katika uchumi wa visiwa hivyo. 

Majanga ya asili yamesababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani :ripoti

Miaka 20 iliyopita imeshudia  ongezeko la asilimia 151 ya hasara ya kiuchumi ya moja kwa moja  kote duniani kutokana na majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, imesema ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa .

Rwanda, Kenya na Côte d’Ivoire kidedea ripoti ya Benki ya Dunia

Kasi ya  ukuaji uchumi kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ni ndogo kuliko ilivyotarajiwa, imesema ripoti mpya ya Benki ya Dunia kwa mwezi huu wa Oktoba. Siraj Kalyango na ripoti kamili.

Brazil kwanza timizeni haki za binadamu, kubana matumizi kutafuata-UN

Kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka Brazil kutafakari upya mipango yake ya kubana matumizi na kutoa kipaumbele  kwanza kwa haki za binadamu za watu wake ambao wanaathirika na mipango hiyo ya sera za kiuchumi.

Japo uchumi wa dunia unaendelea kuimarika tusibweteke:IMF

Ripoti mpya ya mwelekeo wa uchumi duniani iliyotolewa leo na shirika la fedha duniani IMF inaonyesha kuendelea kuimarika kwa mazingira ya ukuaji duniani lakini pia imebainisha kwamba mzani sawia wa ukuaji huo uko hatarini kuwa hasi.

ECA inaamini usafiri bora wa treni ndio muafaka kwa Afrika

Tume ya kiuchumi kwa ajili ya Afrika, ECA leo imesema inaamini kwamba usafiri wa treni indio utakuwa dawa mujarabu ya kukabiliana na adhya ya usafiri barani Afrika.