Mradi wa mitungi ya gesi kwenye kambi za wakimbizi Tanzania ni mkombozi wa wanawake
Tatizo la ukosefu wa nishati endelevu kwa ajili ya kupikia, limekuwa kikwazo kikubwa kwa jamii ya wakimbizi nchini Tanzania, ambako wanawake na wasichana wamekuwa wakikabiliwa na ubakaji pindi wanapoenda kuokota kuni.