Tunisia

Nimesomea umeme, naanzaje kuwa mfugaji wa kuku?: Mhitimu Chuo Kikuu

Nchini Tunisia, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo duniani, IFAD umeleta nuru kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu nchini humo ambao baada ya kuhitimu wameshindwa kupata ajira na sasa wamejiajiri wenyewe upitia miradi ya ikiwemo ya ufugaji kuku.

Jitihada zaidi zinahitajika kulinda haki ya kukusanyika na kujumuika Tunisia- Mtaalamu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za mikusanyiko ya amani na kujiunga na vyama, Clément Nyaletsossi Voule, ameridhishwa na jitihada za serikali ya Tunisia za kuimarisha demokrasia tangu yalipofanyika mapinduzi mwaka 2011 huku akizisihi mamlaka hizo kuongeza jitihada kulinda haki za mikusanyiko ya amani na kujumuika.

Tuna hofu kubwa baada ya wahamiaji 100 kufa maji Tunisia:IOM

Wahamiaji takriban 100 wamekufa maji, 68 kunusurika na wengine hawajulikani waliko baada ya boti yao kuzama mwambao wa Kerkennah-Sfax nchini Tunisia mwishoni mwa wiki.