Kutoka uchuuzi wa karanga hadi kusafirisha China
Jukwaa la kimataifa la kuchagiza biashara ya nje likikunja jamvi hii leo huko Lusaka nchini Zambia, kijana mmoja mjasiriamali kutoka Gambia ameelezea jinsi ambayo ameweza kukuza biashara yake ya karanga kutoka uchuuzi wa barabarani hadi kusafirisha nje ya nchi.