Dola 5000 zamsubiri mshindi wa uhifadhi wa mazingira Tanzania
Wakati nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP25 wakikutana huko Madrid, Hispania, nchini Tanzania mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau wameaandaa maonyesho ya siku mbili yatakayoleta pamoja wajasiriamali wanaotekeleza miradi mbalimbali ya kukabiliana au kuhimili mabadiliko ya tabianchi.