TANZBATT-8

Vijana wajitoa kimasomaso kulinda walio taabuni

Kuelekea siku ya walinda amani duniani tarehe 29 mwezi huu wa Mei, tunamulika walinda amani vijana waliojitolea maisha yao ugenini ili kulinda wengine wasio na uwezo wa kujilinda katika nchi zao. Hii ni kwa kuzingatia kuwa ujumbe wa mwaka huu ni Kuelekea amani ya kudumu: Matumizi ya nguvu ya vijana kwa ajili ya amani na usalama.

Juhudi za UN kurejesha amani zapongezwa DRC

Shughuli za ulinzi wa amani zinazofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO na jeshi la serikali ya DRC, zimepongezwa na viongozi wa dini pamoja na wananchi wa mji wa Mutwanga ulioko katika eneo la Rwenzori jimboni Kivu Kaskazini.

Askari walinda amani wanawake kutoka Tanzania wawatembelea wanawake Beni, DRC

Kikundi cha walinda amani wanawake kutoka Tanzania katika kikosi cha nane kinachohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa FIB MONUSCO, nchini DRC, kimewatembelea wanawake wa kata za Matembo, Nzuma na Ngadi wilaya ya Beni. 

Kikosi cha 8 cha Tanzania cha kulinda amani, TANZBATT-8 chawasili DRC na mipango madhubuti.

Kikosi cha 8 cha Tanzania, TANZBATT-8 kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO.