TANZBATT-8

Juhudi za UN kurejesha amani zapongezwa DRC

Shughuli za ulinzi wa amani zinazofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO na jeshi la serikali ya DRC, zimepongezwa na viongozi wa dini pamoja na wananchi wa mji wa Mutwanga ulioko katika eneo la Rwenzori jimboni Kivu Kaskazini.