Tunaondoka DRC tukiwaachia usalama katika maeneo ambayo yalikuwa hayapitiki - TANZBATT 8
Kikosi cha 8 cha wanajeshi kutoka Tanzania, TANZBATT 8 ambacho kimekamilisha muda wake wa kuhudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, kimesema kinajivunia kuondoka nchini humo kikiwa kimesaidia kuleta amani katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo ya barani Afrika ambayo imegubikwa na mizozo kwa muda mrefu.