Tanzania

Miongozo ya utalii imetuwezesha kushinda tuzo na utalii umerejea Tanzania – TTB

Wakati janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 likiendelea kusababisha zahma kwingineko duniani na hata kukwamisha shughuli za kiuchumi na kijamii, nchini Tanzania hali ni tofauti na kutokana na kuzingatia kanuni za kulinda wananchi na watalii, shughuli za utalii zimerejea na hata taifa hilo la Afrika Mashariki limepata tuzo ya Mhuri wa kimataifa. 

Mbio za Selous zachagiza uhifadhi wa mazingira na utalii

Nchini Tanzania, Umoja wa Mataifa umesema utaendelea kushirikianana serikali katika kuhifadhi mazingira sambamba na kuhakikisha kuwa uhifadhi huo unachangia katika kuongeza kipato kwa wananchi. 

Tumedhamiria kupunguza pengo la kijinsia katika tasnia ya upigaji picha Tanzania-Nsamila

Nchini Tanzania, mpiga picha maarufu, Imani Nsamila, kwa kushirikiana na shirika la Ladies Joint Forum na Kikoi innovative media, wamewapa mafunzo ya upigaji picha wasichana 28 ikiwa ni moja ya harakati za kuchangiakuyafikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs, kama vile lengo namba 5 linalolenga ulimwengu kuwa na usawa wa kijinsia kufikia mwaka 2030. 

Kutotegemea misaada ya kigeni kumewezesha Tanzania kuingia uchumi wa kati-UN

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milišić amesema kitendo cha taifa hilo la Afrika Mashariki kutotegemea misaada ya kigeni ni miongoni mwa sababu zilizowezesha kuingia katika uchumi wa kati. 

Mchango wa vijana kuleta mabadiliko Tanzania ni mkubwa:Restless Development

Katika kuelekea siku ya vijana duniani itakayoadhimishwa 12 Agosti juma hili ni bayana kwamba vijana kila kona bado wanakabiliwa na changamoto lukuki na mara nyingi mchango wao wa kuleta mabadiliko ama hauonekani au unapuuzwa, lakini sasa hatua zinachukuliwa kubadili hali hiyo ikiwemo nchini Tanzania.