Tanzania

WFP na serikali ya Tanzania kushirikiana kuwainua wakulima na wanaohitaji msaada wa chakula

Serikali ya Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula diuniani WFP, wameafikiana kuhusu ubia ambao utawanufaisha wakulima wadogo wadogo wa Tanzania na maelfu ya watu wanaohitaji na kupokea msaada wa chakula  wa WFP barani Afrika.

Licha ya hatua zinazochukuliwa ukatili wa kijinsia bado mtihani Tanzania

Ukatili wa kijinsia hususan kwa wanawake na watoto unaendelea kutoa changamoto kubwa nchini Tanzania.

Watoto wetu, tunu yetu tuwape elimu inayostahili:Tanzania

Wiki ya elimu Tanzania inaadhimishwa juma hili ikibeba kauli mbiu “uwajibikaji wa pamoja katika kutoa elimu bora, watoto wetu tunu yetu”, madhumini ni kuchagiza ufikiaji wa lengo namba 4 la maendeleo endelevu SDG’s lihusulo elimu.

Uelewa wa usawa wa jinsia wabadili maisha ya kaya Ruvuma nchini Tanzania

Ainisho la suala la usawa wa kijinsia limekuwa likileta utata hasa pale ambapo jamii haijaweza kushirikishwa vyema kutambua manufaa ya suala hilo. Huko wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma nchini Tanzania,  suala hilo ambalo ni lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs sasa limeanza kushika kasi.

Nchi nyingi zataja ukosefu wa takwimu sahihi kuwa kikwazo cha kufanikisha SDGs

Mwezi Julai ni mwezi wa mapitio ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs , malengo ambayo ni ahadi iliyoridhiwa na mataifa 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015.

Utoro usipodhibitiwa lengo la elimu itakuwa ndoto Tanzania:

Utoro mashuleni ni moja ya tishio kubwa la kutotimiza lengo namba nne la maendeleo endelevu lihusulo elimu kama hautodhibitiwa nchini Tanzania. Sasa serikali imeamua kulivalia njuga sula hilo kwa kampeni ya mkoa kwa mkoa na mkono wa sheria.

Pedi za Elea ni mkombozi kwa wasichana na wanawake- Bi. Shigoli

Harakati za kuona kuwa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs unagusa maisha ya kila siku ya wananchi hususan wale wa pembezoni na kipato cha chini zinaendelea kushika kasi, na harakati zilizozaa matunda hivi karibuni ni ubunifu wa pedi za kike ambazo zatumika tena na tena huko Tanzania.