Tanzania

29 OKTOBA 2019

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Arnold Kayanda anakuletea

-Mafuriko yameighubika Pembe ya Afrika, shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA na wadau wengine wanahaha kuwasaidia maelfu ya waathirika Sudan kusini, Somalia na Ethiopia.

Sauti -
12'14"

Jukumu la wanawake walinda amani kwenye mizozo ni zaidi ya kubeba mtutu- Tanzania

Mkutano kuhusu wanawake amani na usalama ukifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani na kuleta shuhuda za wanawake walinzi wa amani na uzoefu wao kwenye uwanja wa mapambano hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Tanzania imesema uzoefu huo ni ushahidi tosha kuwa jukumu la wanawake kwenye ulinzi wa amani ni zaidi ya kubeba mtutu wa bunduki.

25 Oktoba 2019

Katika jarida letu la mada kwa kina hii leo Grace Kaneiya anakuletea

Sauti -
9'56"

Tunaushukuru Umoja wa Mataifa kwa kutuwezesha Tanzania:Wananchi

Kwa miaka 74 Umoja wa Mataifa umekuwa na mchango mkubwa kote duniani katika njanja mbalimbali ikiwemo kudumisha amani, maendeleo na hata msaada kwa walio na uhitaji mkubwa. Na je walengwa wa Umoja wa Mataifa ndivyo wanavyohisi kuhusu Umoja huo? tuwasikilze wananchi hawa kutoka Tanzania.

Sauti -
2'10"

Wasichana wa Tanzania leo wamepata ushindi mkubwa dhidi ya ndoa za utotoni:Gyumi

Mahakama kuu nchini Tanzania leo imesimamia hukumu yake ya awali kwamba vifungu vya Sheria ya ndoa ya nchi hiyo vinapingana na Katiba kwa kuweka umri tofauti wa kuoa au kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume.

Sauti -
2'48"

Ubunifu wa spika janja Kaya sasa kuanza kuingia sokoni mwakani

Kila uchao Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushiriki wa vijana katika kuleta mabadiliko katika dunia ya sasa na kuhakikisha mustakabali wa kizazi kijacho unakuwa bora.

Sauti -
4'26"

Ushindi huu ni kwa Watoto wote wa kike Tanzania:Gyumi

Mahakama ya rufaa  kuu nchini Tanzania leo imekazia hukumu ya mahakama kuu nchini humo kwamba vifungu vya Sheria ya ndoa ya nchi hiyo vinapingana na Katiba kwa kuweka umri tofauti wa kuoa au kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Na hivyo kuitaka serikali kubadili sheria hiyo ambayo ni baguzi kwa watoto wa kike ndani ya mwaka mmoja.

23Oktoba 2019

Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Grace LKaneiya anakuletea

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J.Mohammed amesema mchango wa wanawake Somalia katika masuala ya amani ni muhimu na wa lazima kwa ajili ya mustakabali wa taifa hilo

Sauti -
12'5"

Tuligundua kwa kukuza uchumi wa mwanamke, tutakuza uchumi wa jamii nzima-Paul Siniga

Asasi ya African Reflections Foundation inayojishughulisha na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs nchini Tanzania, kwa miaka mingi imejikita katika kuleta usawa wa kijinsia nchini humo kwa njia ya kukuza ushiriki wa shughuli za uchumi kwa wanawake.

Sauti -
3'15"